KUWACHA TABIA YA KUWEKA MAKUNDI KATIKA SEHEMU ZA KAZI

 

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini ‘B’ Bw: Makame Mwadini Silima amewashauri wafanyakazi wa halmashauri hiyo kuwacha tabia ya kuweka makundi katika sehemu za kazi na badala yake kushirikiana ili kufanyakazi kwa ufanisi

Akizungumza na wafanyakazi hao huko kinduni amesema lengo la halmashauri ni kuhakikisha wanafikisha kwa wakati huduma muhimu kwa wananchi wanaowaongoza hivyo ili kufikia lengo hilo ni vyema watendaji kushirikiana pindi wakiwa kazini ili kutoa huduma bora.

Amefahamisha kuwa serikali inawapenda sana watendaji wake lakini pia haitomvumilia mfanyakazi yeyote atakae kwenda knyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw: Ame Simai Daima amewaasa watendaji hao kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha wanazuia mianya ya upotevu wa mapato kwani kufanya hivyo wataweza kuwatumikia vizuri wananchi na kutatua matatizo yanayowakabili kupitia sekta ya afya,kilimo na elimu