KUWAHAMASISHA WANANCHI KUCHANGIA DAMU ILI KUSAIDIA WANANCHI WANAOHITAJI

Viongozi wa serikali, na kijamii wametakiwa kuitumia nafasi zao kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ili kusaidia wananchi wanaohitaji ikiwemo mama wajawazito na majeruhi wa ajali.
Meneja wa benki ya damu zanzibar dk mwanakheir ahmed amesema upatikanaji wa damu unategemea na ushawishi wa viongozi hao wa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia damu katika kulinda maisha ya wananchi.
Dk mwanakheir ametoa wito huo kwenye hafla ya ufunguzi wa kituo cha benki ya damu kisiwani pemba na kusema kuwa uwepo wa damu ya kutosha katika benki hiyo utasaidia sana akinamama wajawazito pale wanapohitaji huduma hiyo.
Naye katibu tawala mkoa wa kaskazini pemba ahmed khalid abdalla akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo , amesema serikali ya mkoa itaendelea kuwahamasisha wananchi ili watambue umuhimu wa kuchangia damu .