KUWAIT IMEIHAKIKISHIA ZANZIBAR KUENDELEA KUIUNGA MKONO

 

Serikali ya kuwait imeihakikishia serikali ya mapinduzi zanzibar kuendelea kuiunga mkono katika harakati zake za kuimarisha miradi ya maendeleo na ustawi wa wananchi.

Hatua hiyo itakwenda sambamba na mpango wa maalum uliobuniwa na ofisi ya ubalozi wa kuwait nchini tanzania wa kusaidia vifaa na zana za kisasa zitakazowawezesha watu wenye ulemavu  kutengeneza vitu vya sana vyenye viwango vya ubora.