KUWEKEZA ILI KUWEZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI KIUCHUMI

 

Mkuu  wa  mkoa  mjini  ‘magh’i  mh  ayoub  muhamed  mahmoud  amewataka  wawekezaji wa nishati  mbadala  kuja nchini kuwekeza   ili kuweza   kuongeza  kasi  ya  uzalishaji  kiuchumi pamoja na  kuondokana na umeme  wa  utegemezi kianzio kimoja.

Akizungumza  katika  mafunzo  kwa  viongozi  wa  serikali   za  mitaa  na  viongozi  wa  dini kuhusu  umuhimu wa  nishati  mbadala   nchini  ayoub  amesema kuwepo  kwa  njia  mbadala  ya upatinaji  umeme  kutasaidia  kupunguza  gharama  kwa  wananchi  na kuchochea harakati   kiuchumi.

Amefahamisha  kuwa serikali  imeandaa  utaratibu  maalum kwa  mujibu  wa  tafiti  zinazoendelea  kufanyika  kwa  kuweka  sera  zitazoleta  tija  ambapo   kutakakowafanya  wawekezaji  kuzingatia taratibu  zilizopo  ili  kupunguza  ukali  wa  maisha  kwa  wananchi  wake.

Mkurugenzi  wa  idara  nishati  nd  muhammed  abdalla  muhamed  amesema    tafiti  zinaonyesha  matokeao  mazuri  ya kuhusiana na  umeme  wa  jua   hivi  sasa  serikali  ipo  katika  harakati  za  kukamilisha taratibu  za  ki sera  na   kisheria ili  kuweza  kuwekeza.

Kuhusu umeme wa  njia  ya  upepo  wataalamu  wameshauri  kuendelea  kukusanywa  takwimu  kwa  kipindi  cha  mwaka  ili  kuweza  kupata matokeo  sahihi  ya  mara  ya  pili.

Msaidizi wa  mradi  nishati  mbadala  nd  omar saleh amesema   hivi  sasa  zanzibar  inatumia  kiwango  kikubwa  cha  umeme  kufikia  megawat 68 wakati  waya  uliopo  unachukuwa  megawat  100  kwa  matumizi  ya  nchi  nzima  hivyo  ipo  haja  ya  kutafuta na  kutumia  njia  mbadala  ili  kujinusuru  na matumizi  ya  umeme  wa  mgao  nchi  nzima.