KUWEPO ADHABU MBADALA YA ADHABU YA KIFO KUTAWEZESHA BINADAMU KUPATA HAKI ZAO ZA MSINGI

Katibu tawala wilaya ndogo ya tumbatu nd, khatib habibu ali amesema kuwepo adhabu mbadala ya adhabu ya kifo kutawezesha binadamu kupata haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya adhabu ya kifo duniani yaliyofanyika tumbatu uvivini, katibu huyo amesema adhabu hiyo imekuwa ikiathiri jamii kisaikolojia .
Nae afisa mipango kituo cha huduma za sheria zanzibar bw, thabit abdalah juma amesema lengo la maadhimisho hayo kwa hapa zanzibar ni kuishawishi serikali kuondosha adhabu ya kifo kwani sheria hiyo inakwenda kinyume na mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu
Aidha wananchi wa tumbatu wameshukuru kituo cha huduma za sheria kwa kuwapelekea elimu hiyo na kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa kufuta adhabu ya kifo.