KUWEPO KWA MASHIMO KATIKA KIJIJI CHA PANGATUPU

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha pangatupu wamelalamikia kuwepo kwa mashimo katika njia inayopita daraja la kuelekea kijiji cha mwanza ndogo na kusababisha usumbufu wakati wa mvua hasa kwa kina mama na watoto
Wanachi hao wamesema licha ya kuwepo daraja katika njia hiyo lakini kunakuwepo na usumbufu mkubwa kwani mashimo yaliopo katika njia hiyo yanajaa maji na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano baina ya wananchi wa kijiji cha pangatupu na mwanza ndogo pamoja na kukosekana kwa huduma muhimu ya chakula
Mwakilishi wa jimbo la bubwini mh:mtumwa pea yussuf amefanya ziara katika njia hiyo na kuwataka wananchi wa vijij hivyo kuwa wastaamilivu na kuahidi kulitatua tatizo hilo kabla ya halijaleta athari
Wakati huo huo mh: mtumwa amewataka wananchi wa bumbwini bwaga kuwa waangalifu katika shimo lilojitokeza na kusema kuwa atafanya mawasiliano na idara ya mazingira ili kulifukia shimo hilo ambalo hadi sasa linaleta wasiwasi mkubwa kwa wakaazi wa karibu na eneo hilo