KUWEPO KWA UTAMADUNI WA KUWAKAGUA NA KUWATEMBELEA WAASISI WA CHAMA CHAMAPINDUZI

 

kuwepo  kwa  utamaduni  wa  kuwakagua  na  kuwatembelea  waasisi  wa  chama  chamapinduzi  ni  njia  moja  wapo  ya kupata  kujifunza  kwa  jumuiya  za  chama  ili  ziweze  kuleta  ufanisi katika utekelezaji  wa  kazi  zao.

hali  hiyo  imebainishwa  na  viongozi  wa  jumuiya   ya  vijana  wa  Ccm wa wilaya  mfenesini  katika  kuwatembelea  waasisi  wa  chama  hicho  ambao  walikitumikia kwa  kipindi  kirefu na kutoa  mchango  mkubwa  ndani  ya  chama  na  jumuiya  zake.

wamesema vijana  hao kuwa   waasisi  hao  wataendelea  kuwaenzi   huku  wakithamini  jitihada  kubwa  walioichukua  katika  kuikomboa  nchi na  kubaki  katika  mazingira  ya amani  na  utulivu  nchini.

nao  waasisi  hao  wameshauri  kufanyika  ukaguzi  wa  kadi  za  wanachama  ili  kubaini  waliohai  na kuendelea  kuhamasisha  uingizaji  wa  wanachama  wapya  na  kuzilipia  kadi  zao  ili  kuweza kufikia  malengo  ya  chama  chao.

miongoni  mwa  waliotembelewa  na  jumuiya  hiyo  akiwemo  Nd Hassan  Omar  mkele  aliechanganya mchanga  wa  Zanzibar  na  Tanganyika   na  kuwa  Tanzania amesisitiza  vijana  kujifunza  historia  ya  nchi  ili  kuweza  kuwa  wazalendo  wa  nchi  yao.