KUWEPO KWA WALIMU WAZURI WA KUFUNDISHA KUTASAIDIA KATIKA KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUFAHAMU MASOMO VIZURI .

Kuwepo kwa walimu wazuri na wenye uwezo mkubwa wa kufundisha wanafunzi masomo ya sayansi kutasaidia katika kuwawezesha wanafunzi kufahamu masomo yao kwa vizuri .
Hayo yameelezwa na bi khadija ahmed sharif kutoka milele foundation katika uzinduzi wa mradi wa kuwawezesha wanafunzi wa kike katika ukumbi wa maru maru forodhani.
Amesema mradi huo unalengo la kuwawezesha wanafunzi wa kike kubadilika mitazamo yao ya kielimu na kuweza kujua wapi wataelekea katika maisha yao .
Akizindua mradi huo dr mwatima abdallah juma m/kiti wa fawe zanzibar amesema ili wanafunzi wafahamu vizuri lazimza walimu watumie njiatofauti za kufundishia.
Kwa upande wake dr maryam jaffar ismail kutoka suza amesema kupitia mradi huo wataandaa mitaala mizuri itakayowawezesha walimu kufundisha kitaalamu.
Mradi huo wa miaka2 utaendeshwa kwa ushirikiano wa chuokikuu cha zanzibar suza ,fawe zanzibar na milele foundation na utajumuisha skuli 15 za serikali unguja na pemba.