KUWEPO NA UTAMADUNI WA KUJITOLEA HASA KATIKA MAMBO YA KIJAMII

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema maendeleo yataendelea kupatikana endapo jamii itarejesha utamaduni wa kufanya kazi za ujenzi wa taifa kwa kujitolea hasa katika maeneo ya huduma za kijamii.

Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Mh. Ayoub mohamed mahmoud amesema hatua hiyo ni kuunga mkono kampeni ya mimi na wewe ilokusudia kujenga madarasa 50 katika mkoa huo ili kupunguza tatizo la madarasa katika skuli za mkoa huo.

Akizungumza katika ujenzi wa taifa katika skuli ya msingi na sekondari ya kijitoupele amesema ushirikiki wa wananchi katika ujenzi huo umempa faraja na utasaidia kutatua matatizo ya wananchi kwa ushirikiano.

Kaimu kamishna wa mamlaka ya bima tanzania nd juma juma makame na uongozi wa shirika hilo kanda ya zanzibar ni miongoni mwa wadau waliomuunga mkono mkuu wa mkoa kwa kushiriki  ujenzi wa taifa na kuchangia mabati 62 huku wakiahidi kuendelea kushirikiana kufanikisha kampeni hiyo.

Kampeni ya ujenzi wa madarasa ni endelevu kwa maeneo mbali mbali ya mkoa wa mjini magharibi ambapo siku ya jumamosi utaendelea katika skuli ya sharifumsa