KUYAFANYIA UTAFITI MAENEO YA MICHEWENI GININGI ILI KULIMWA ZAO LA KOROSHO.

Waziri wa klimo maliasili mifugo na uvuvi mh. Hamad rashid mohamed ameiagiza wizara ya kilimo pemba kushirikiana na idara ya misitu kuyafanyia utafiti maeneo ya micheweni giningi ili kulimwa zao la korosho.
Amesema sehemu hizo zina maeneo makubwa yanayoonyesha zao hilo linauwezo wa kustawi vizuri na kuweza kutoa ajira kwa wananachi wengi
Mh waziri ametoa agizo hilo huko giningi wilaya ya mkoani wakati akiangalia eneo hilo lililokuwa linatumiwa kuchimba mchanga .
Ameongeza iwapo wizara itaufanyia kazi mpango huo utasaidia pia serikali kuingiza mapato kwa zao hilo badala ya kupanda miti isiyo na faida .
Wakati huo huo mh rashid amezindua gari la uvunaji wa zao la mpunga pujini na kuangalia kilimo cha zao la alizeti pamoja na mashine ya kukamulia mafuta ya zao hilo huko kituo cha kilimo na utafiti dodeani ole.
Nao baadhi ya wakulima hao wamesema kuwepo kwa gari hiyo kutawasaidia kuvuna kwa haraka pia kupata mazao yao katika katika hali bora.