KUZIIMARISHA IDARA MAALUM ZA SMZ ILI ZITEKELEZE MAJUKUMU YAKE KWA UFANISI ZAIDI.

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema itasimamia dhamira yake ya kuziimarisha idara maalum za smz ili zitekeleze majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Waziri wa nchi ofisi ya raisi,tawala za mikoa,serikali za mitaa na idara maalum za smz  mh haji omar kheri akizungumza na maafisa wa vikosi vya zimamoto na uokozi na kikosi maalum cha kuzuia magendo kmkm amesema  miongoni mwa hatua hizo ni kutatua matatizo yanayokwamisha utendaji wa vikosi hivyo ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake .

Amesisitiza   kuwa  serekali itarekebisha sheria  ambayo itawalazimisha vijana wote wanaomaliza masomo  wajiunge na jku kabla ya kuajiriwa  ili kuwajengea uzalendo,elimu ya amali na kupata muamko wa kudumisha amani na utulivu wa taifa.

Wakuu wa vikosi hivyo wameahidi kuongeza ari ya kujituma na kushirikiana katika kutekelezaji dhamana zao kwamaslahi ya nchi.