KUZITHAMINI NA KUZITUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA KUTENGENEZWA NCHINI

 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini unguja mhe: Hassan Hatibu Hassan amewataka wananchi kuzithamini na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na kutengenezwa hapa nchini ili kuinua soko na maendeleo hasa kwa wanawake nchini.

Akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 51 wanawake wa kikundi cha hapa kazi tu cha shehia hiyo mhe khatibu amesema katika kuunga mkona juhudi za wajasiriamali wa mkoa   huo serekali ya mkoa  huo inakusudia  kutafuta eneo malum la kuanzisha  soko la  pamoja  la kuuzia  bidhaa za wajasiriamali hivyo amewataka kuzalisha  bidhaa zenye  ubora ili kukabiliana  vyema na ushindani wa kibishara.

Nae m/kiti wa ccm tawi hilo ndugu said kheri mtumwa  amesema lengo  la kufanyika kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo vijana waweze kujikwamua kiuchumi  na  kukabiliana  na tatizo la ajira kwa  vijana.

Nao wanakikundi hao wamesema pamoja na mafanikio wanayoyapata lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi.