KUZUIA MATUMIZI MABAYA NA KINYUME CHA SHERIA ZA UMILIKI WA ARDHI

 

Mkoa wa Mjini Magharibi umebaini meneo kiasi ya heka   eka 120 ambazo wamiliki wake wamekiuka masharti ya matumizi  na kuchukuwa hatua  kama ilivyofanya huko shehia ya kianga hivi karibuni.

Umeeleza kuwa hatua itakazozichukuwa ni kuzuia matumizi yote ya kinyume cha sheria za umiliki wa ardhi hizo ikiwemo  kubomoa majengo na baadae kuzirejesha eka hizo serikalini kwa ajili ya kuendelezwa kwa shughuli za kilimo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud  Amefahamisha kuwa kwa mujibu wa mpango mkuu wa matumizi ya ardhi ulotiwa saini hivi karibuni maeneo hayo yametengwa kwa shughuli za kilimo na mengine ni vianzio vya maji lakini wananchi wasiokuwa waaminifu wameyavamia na kuuza kwa ajili ya makaazi  kinyume na taratibu.

Akizungumzia kuhusu ubomoaji wa nyumba zilizojengwa katika maeneo ya Eka Shehia ya kianga umefanyika kwa mujibu wa   sheria ya matumizi ya ardhi ya mwaka ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na haina nia ya kuwaonea wananchi.

Jumla ya nyumba 74 zilibomolewa katika maeneo ya Kianga Sharkia kufuatia agizo lililotolewa na serikali baada ya kubainika wananchi kuvamia katika maeneo hayo ambayo yametengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na vianzio vya maji