LESENI 225 ZA MADEREVA AMBAO WASIO NA VYETI ZAKAMATWA

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani nchini limekamata na kuzuia leseni 225 za madereva ambao wasio na vyeti vinavyothibitisha kuhitimu taaluma ya udereva.

.akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani (sacp) fortunatus musilimu amesema hatua hiyo imekuja kufuatia oparesheni kali inayoendelea kufanywa na jeshi hilo kwa lengo la kukagua leseni za madereva, vyombo vya moto na kutoa elimu juu ya usalama barabarani  kwa makundi mbalimbali ya watumia barabara.

Amesema oparesheni hiyo inaongozwa na kusimamiwa na makamanda wa polisi wa mikoa ambapo hadi sasa jumla ya leseni 73,904 za madereva zimekaguliwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 4 hadi 15 mwezi huu wa saba ambapo pia wamebaini madereva kuendesha magari wakiwa na madaraja yasiyostahiki.

Aidha kamanda musilimu amesema zoezi hilo limesaidi kupunguza ajali za barabarani,         up-sound

Kwa upande wa ukaguzi wa vyombo vya moto kamanda musilimu amesema jumla ya vyombo 81,533 vimeweza kukaguliwa na kuyabaini magari 33,637 kuwa ni mabovu

Huku pia likisema kuanzia agosti mosi mwaka huu watafanya uhakiki wa kina wa leseni kwa madereva nchini