LIBYA WAMEFANIKIWA KUWAREJESHA ZAIDI YA WAHAMIAJI 150

Walinzi wa pwani nchini libya ambao wanasaidiwa na umoja wa ulaya jana wamefanikiwa kuwarejesha zaidi ya wahamiaji 150 ambao walikuwa wakijaribu kuingia italia kwa kutumia usafiri wa boti katika kipindi hiki kukiwa na jitihada kali zaidi za kuzuia safari hizo za hatari za kuvuka bahari ya mediterranean. Wahamiaji hao walikuwa katika boti moja, pale walipozuiwa katika fukwe, kati ya miji ya al khoms na garabulli, mashariki mwa tripoli, wakiwa tayari wamesafiri usiku kucha. Idadi kubwa ya wahamiaji hao walikuwa kutoka matiafa ya afrika magharibi ambayo ni mali, guinea, na nigeria, na baadhi kutoka bangladesh. Wote isipokuwa mmoja walikuwa wanaume.