LORRY MOJA LA MIZIGO JAMHURI YA AFRIKA YA KATI CAR LIMESABABISHA AJALI NA KUUWA ZAIDI YA WATU 80

Lorry moja la mizigo jamhuri ya Afrika ya Kati Car limesababisha ajali na kuuwa zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa wakielekea sokoni mjini Bambari.

walioshuhudia tukio hilo wamesema Lorry hilo lilikuwa limebeba watu wengi na kujazwa mizigo kupita uwezo wake huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi wakati lilipopenduka.

maafisa wa usalama wa barabarani wamelaumiwa kwa kutochukua hatua za kuzuia ukiukwaji huo wa sheria za barabarani.

ajali kama hii zimekua zikitokea, katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi, ambapo polisi inanyooshewa kidole kwa kujihusisha na rushwa.