MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI

Wizra ya afya imesema tatizo la maradhi ya afya ya akili bado ni tatizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo na matumizi ya dawa za kulevya.
Katibu mkuu wizara ya afya bi asha abdalla amesema ongezeko hilo pia limo katika sehemu za makazi ambapo takwimu zinaonyesha kati ya wafanyakazi sita mmoja anaugua maradhi ya afya ya akili.
Katibu mkuu huyo alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani ambapo amehimiza kwa waajiri kusaidia kutatua matatizo ya wafanyakazi ili waondokane na msongo wa mawazo.
Nao wafanyakazi walioshiriki katika maadhimisho hayo wamesema kumekuwa na matatizo mengi katika maeneo ya kazi hali inayohitaji ufumbuzi na kushauri kuanishwa vituo vya ushauri nasaha katika taasisi mbalimbali.
Nae mbunge wa jimbo la magomeni amewahimiza vijan a kujitambua ili kuepukana na matatizo ambayo yanachangiwa na matumzii ya dawa zakulevya.