MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Kukosekana sheria maalumu ya usimamizi wa rasilimali ya misitu kunasababisha kuongezeka kwa ukataji wa misitu siku hadi siku.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa waandishi a habari mwenyekiti wa jumuiya ya mabadiliko ya tabianchi zacca amina yusuf amesema utafiti uliofanywa na idara ya misitu uanonyesha kuwa zanzibar inapoteza hekta miatano mwaka kutokana na kutokuwepo na udhibiti mzuri wa kuapmbana na ukataji wa miti ovyo.
Amesema licha ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar na asasi za kiraia kuchkua juhudi za makusudi za kuhakikisha wanapambana na mabadiliko ya tabianchi lakini bado kumekuwa na kasi ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ovyo, uchimbaji wa mchanga na utupaji wa takataka ovyo.
Aidha ameishauri serikali kuweka sheria ya za mtu atakayehusika na uharibufu wa mazingira achukuliwe hatua kali ili kufikia wakati kukabiliana na mabadiliko hayo.
Wakielezea hali halisi ya mabadiliko mratibu na waakazi wa maeneo mbalimbali wamesema kuwa elimu zaidi inahitajika kwa jamii katika kupambana na athari za mabadiliko hayo.
Hata hivyo wamewataka wananchi kuchukua tahadhari ya uharibfu wa mazingira kwani hunasababisha mafuriko na majanga mbalimbali kutokea