MAAFISA KUTOKA IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU WAMETAKIWAA KUFANYA KAZI KWA UWELEDI

 

Maafisa  kutoka idara ya watu wenye  ulemavu wanaokwenda kufanya zoezi la usajili wa watu wenye ulemavu hasa wenye ulemavu mkubwa wametakiwaa kuifanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa ili kuweza kufikia lengo na serikali lililokusudiwa.

naibu waziri wa nchi wa afisi ya makamu wa pili wa raisi muheshimiwa Mihayo Juma Nunga ameyasema wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maafisa kutoka idara ya watu wenye ulemavu watakaokwenda kufanya usajili wa watu wenye ulemavu katika mkoa wa kusini unguja yaliyofanyika  katika ukumbi wa  tume ya uchaguzi maisara.

aidha muheshimiwa mihayo amesema zoezi la usaji wa watu wenye ulemavu linachangamoto mbali mbali hasa vijijini na kuwataka kutumia busara pamoja na lugha nzuri ili kuona watu wote wenye ulemavu wanasajiliwa na kupata haki zao stahiki.

mkurugenzi wa idara ya watu wenye ulemavu  bi abeda rashid amesema idara imeanzisha kamati za watu wenye ulemavu kwa baadhi ya shehia ambazo zimejumuisha wajumbe kumi ili kuweza kupata taarifa za ukweli na uhakika za watu wenye ullemavu.

mshiriki wa mafunzo hayo abushiri said khatib ametoa wito kwa washiriki wenziwe kwenda kuifanya kazi ya usajili kwa moyo wa kujitolea ili kuweza kutimiza lengo la serikali.

mada mbili zimewasilishwa katika mafunzo hayo ikiwemo uwasilishaji wa dhana ya ulemavu kwa ujumla ikiwemo ulemavu mkubwa na uwasishaji wa vigezo vya ulemavu mkubwa.