MAAFISA WA TEHAMA WANATAKIWA KUTUMIA VYEMA TAALUMA YAO

 

Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais katiba sheria, utumishi wa umma na utawala bora Seif Shabaan Mwinyi amesema maafisa wa tehama wanatakiwa kutumia vyema taaluma yao katika kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maafisa wa teknolojia ya habari ya mawasilianio wa taasisi za umma yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Rais katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora mazizini, wilaya ya magharibi b.

Amesema ni muhimu kwa maafisa wa tehama kuwa na mpango mkakati wa utendaji kazi, ili kuweza kuitumia vyema idara ya serikali mtandao ambayo lengo lake ni kuimarisha utumishi wa umma na utawala bora.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ndugu Rafael rutahiwa ambae ni mwanasheria wa serikali mtandao tanzania bara amesema matumizi ya tehama ni mpango wa   kutoa huduma kwa umma ambao unarahisisha kupatikana kwa huduma na  taarifa kwa gharama nafuu kutoka serikalini kwenda kwa wananchi.

Nae mkurgenzi wa serikali mtandao Zanzibar ndugu Shaban Haji Chum amesema Teknolojia ya habari na mawasiliano itarahisha utamuwezesha mwananchi kupata huduma mahali alipo na kufanya malipo bila kufika katika taasisi husika.