MAAFISA WADHAMINI KUWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAO WANAPOSTAAFU

 

Mkuu wa mkoa wa kusini pemba mh: hemed suleiman abdalla amewataka maafisa wadhamini     kuwapa motisha wafanyakazi wao wanapostaafu kwa ajili ya  kuthamini mchango  waliotoa katika  taasisi zao .

Mh: hemed ametoa kauli hiyo huko ukumbi wa baraza la mji chake chake katika hafla ya kumuaga na kumkabidhi  zawadi  aliyekuwa afisa mdhamini afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi  bi jokha khamis makame  baada yakumaliza muda wake wa utumishi wa umma.Mkuu huyo wa mkoa amesema katika utumishi wake bijokha alitoa mchango mkubwa kuwaelekeza watendaji pamoja na kuwakosoa pale ambapo kulikuwa na kasoro za maadili ya  kiutendajii.

Nae afisa mdhamini afisi ya makamo wa pili wa rais ali salim mata   kwa niaba ya maafisa wadhamini amesema bado wataendelea  kushirikiana nae katika kufuata nyendo zake  na    kujipanga upya  ili kutekeleza  vyema majukumu yao.Akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo   bi jokha   amewataka viongozi hao kufanya uadilifu katika kwatumikia wananchi.