MAAFISA WATAKAOINGIA KATIKA MPANGO WA UGATUZI KUWA TAYARI KUUPOKEA MPANGO HUO

Mkuu wa moa wa kusini pemba mh. Mwanajuma majid abdalla amewataka maafisa watakaoingia katika mpango wa ugatuzi wa madaraka kuwa tayari kuupokea mpango huo na kufanya kazi kwa uwezo wao kikamili.
Akifungua mkutano wa kujadili mpango huo kwa maafisa kutoka sekta mbali mbali za serikali ya mapinduzi zanzibar ,katibu tawala wa mkoa huo ndugu yussuf mohammed ali kwa niaba ya mkuu wa mkoa kusini pemba amesema kuondolewa kwa maafisa hao kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa haina maana ya kuwashusha hadhi na heshima yao.
Pia ameelezea utaratibu wa muundo wa ugatuzi huo ambapo amesema kutakuwa na sekretariet yenye maafisa watakaopendekezwa ambao watakuwa watendeji wakuu katika sekta zao na kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mapema naibu katibu mkuu ofisi ya rais ,katiba ,sheria utumishi wa umma na utawala bora ndugu seif shaaban mwinyi amesema lengo la mkutano huo ni kupata maoni ya watendaji ili kuamua namna ya kukasimu madaraka.
Jumla ya mada mbili zimewasilishwa katika mkutano huo ikiwemo ya gatuzi wa rasilimali watu na miundombinu ya taasisi na mahusiano ya rasilimali watu ambapo maafisa hao wameshauri serikali kuangalia kwa makini suala la upangaji wa bajeti ambayo itakidhi mahitaji ya utekelezaji mzuri wa mpango wa ugatuzi.