MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa mkoa wa mjini magharib Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kwa mara ya kwanza katika Mkoa wake utakuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru utakao fikia kilele chake OKTOBA 14 Mwaka huu.
Akizungumza na kamati za Mikoa mitatu ya Unguja juu ya MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU kwa mwaka huu amesema Zanzibar imepata heshima ya kipekee na ya kihistoria tokea kuasisiwa kwa mwenge wa uhuru 1961 na kufikia kilele chake hapa Visiwani.
Amefahamisha kuwa katika kilele hicho cha mbio za Mwenge wa uhuru utakaoambatana na kumbukumbu ya Baba wa taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere na wiki ya vijana itakayoanza Oktoba Nane hadi 14.
Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi na viongozi mbali mbali kuungana kwa pamoja katika kuupokea mwenge wa uhuru ambao ni chombo kinachounganisha watanzania kuwa na umoja na mshikamano katika ujenzi wa maendeleo ya nchi.
Nae Mratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Mjini Magharib ndsalama Othman amesema maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge huo umekamilika ambapo lengo kuu la mbio za mwenge wa uhuru ni kuleta ukombozi wa Tanzania na nchi za afrika.
Hata hivyo amesema kama kauli mbili ya mwaka huu unavyosema Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi hivyo amewahamasisha vijana kushiriki katika kazi za ujasiriamali ili kufikia adhma ya serikali ya uchumi wa viwnada.
Mwenge wa uhuru katika Kisiwa cha Unguja utawasili Oktoba saba na utaanza kukimbizwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na baadae kukimbizwa Mkoa wa kusini tarehe 9 na kukabidhiwa Mkoa wa mjini Magharib tarehe 11 ambapo utafikia kilele chake katika mkoa huo katika Uwanja wa Amani .