MAANDAMANO YA KUPINGA UAMUZI WA MAREKANI WA KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL YANAENDE

Maandamano ya kupinga uamuzi wa marekani wa kuutambua jerusalem kuwa mji mkuu wa israel yanaendelea katika mataifa mbali mbali ambapo nchini indonesia maelfu ya watu wameandamana kupinga uamuzi huo.
Maandamano hayo ni hatua ya kuonesha mshikamano na wapalestina katika nchi yenye idadi kubwa zaidi ya waislamu duniani.
Maandamano hayo yameandaliwa na baraza la ulamaa ambalo ni mamlaka kuu ya kiislamu nchini indonesia, na ambalo linaungwa mkono na serikali pamoja na mashirika kadhaa ya kiislamu.
Polisi imesema waandamanaji wapatao elfu 80,000 wameshiriki mjini jakarta huku wakiwa wamebeba bendera ya palestina.
Waziri wa masuala ya kidini nchini indonesia na gavana wa jarkata ni miongoni mwa walioshiriki maandamano hayo, yaliyofanyika mita chache tu kutoka ubalozi wa marekani.
Indonesia imelaani hatua ya trump huku rais joko widodo wa nchi hiyo akiungana na uamuzi ulioafikiwa jumanne wiki iliyopita na wakuu wengine wa kiislamu kwamba mji wa mashariki ya jerusalem utambuliwe kuwa mji mkuu wa wapalestina.