MABADILIKO KWA WANASHERIA KATIKA KUSIMAMIA NA KUHARAKISHA UTOAJI WA MAAMUZI

 

Jaji Mkuu wa Zanzibar mh Omar Othman Makungu amesisitiza mabadiliko zaidi kwa wanasheria hasa katika kusimamia na kuharakisha utoaji wa maamuzi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Ameyasema hayo  wakati wa  mahafali ya kwanza ya chuo cha mafunzo ya sheria zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkurugenzi  wa mashtaka  miembeni.

Mh othman makungu katika hotuba yake kwa wahitimu hao amewataka kuzingatia misingi ya kimaadili ya taaluma yao kwani serikali ya mapinduzi ya zanzibar inahitaji watendaji wenye sifa hizo hususan katika tasnia ya sheria.

Mapema akisoma historia ya chuo hicho  mkuu wa chuo cha mafunzo ya sheria na utafiti zanzibar nd.walid mohammed adam amesema chuo hicho kimeanzia kutoa mafunzo ya muda mfupi kuanzia mwaka 2011 na kuendelea kutoa elimu ya cheti na stashahada kuanzia mwaka 2014 hadi leo.

Nd.walid mohammed adam- mkuu wa chuo cha mafunzo ya sheria na utafiti zanzibar

Sabra othman juma na omary haroub khalid  ni miongoni mwa wahitimu hao wamesema hawanabudi kulitumikia taifa kwa weledi  kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Jumla ya wahitimu 56 wamehitimu mafunzo ya cheti na stashahada na kutunukiwa vyeti vyao.