MABADILIKO NDANI YA CCM HAYAEPUKIKI

 

Mwenyekiti wa ccm taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk. John Pombe Magufuli amewaeleza wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm Taifa kuwa mabadiliko ndani ya ccm hayaepukiki kwani hatua hiyo itakisaidia chama hicho kuimarika zaidi.

Mwenyekiti huyo wa ccm aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao cha halmashauri kuu ya taifa (nec), huko katika ukumbi wa makao makuu ya chama hicho mjini dodoma, ikiwa ni miongoni mwa matayarisho ya mkutano mkuu maalum wa ccm unaotarajiwa kufanyia hapo kesho mjini hapa.

Ameongoza kuwa ccm ni miongoni mwa vyama vikongwe katika bara la afrika na tayari kimeshafanya mambo mengi pamoja na mabadiliko mengi ambayo yamesaidia kukiimarisha chama hicho.

Hata hivyo halmashauri kuu ya taifa ya ccm imechukuwa maamuzi dhidi ya viongozi waliopatikana na makosa ya maadili kinyume na katiba na kanuni za uongozi za ccm ikiwemo kuwafukuza uanachama na wengine kupewa onyo.

Miongoni mwa waliofukuzwa uanachama  mwenyekiti wa ccm mkoa wa iringa jesca msambwatavangu, nd. Erasto izengo kwilasa mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga, ramadhan rashid madabida mwenyekiti wa ccm mkoa wa dar es salaam na christopher sanya mwenyekiti wa ccm mkoa wa mara.

Wengine ni bi sophia simba mwenyekiti wa uwt taifa, josephine genzabuke mwenyekiti wa uwt mkoa wa kigoma amepewa onyo na emanuel nchimbi mjumbe wa kamati kuu ambae amesamehea na ametakiwa aombe radhi