MABADILIKO YA SHERIA MPYA YA CHAKULA ITASAIDIA NCHI KUTOGEUZWA KUWA JAA LA BIDHAA MBOVU.

 

 

Mkurugenzi  mtendaji  wakala  wa  chakula  dawa  na vipodozi  zanzibar   dk  burhan  othman simai  amesema  mabadiliko  ya  sheria  mpya  no 3ya  mwaka 2017   ya  chakula   dawa na  vipodozi  itasaidia  nchi  kutogeuzwa  kuwa  jaa  la bidhaa mbovu.

Akizungumza  na wakala  wa  forodha   na  wafanyabiashara  wa  dawa  chakula  vipodozi  na  vifaa  tiba  amesema   imebainika  kwa  baadhi ya  wafanyabiashara  kukiuka  taratibu   zilizopo   na  kupelekea  kuingiza  nchini  bidhaa  zisizo  naviwango na  kuleta  athari  kwa  mtumiaji.Hivyo  amesisitiza  upo  umuhimu  wa  kusajiliwa  bidhaa  zinazoingizwa  nchini   katika  vyombo  vinavyostahiki ilikuingiza   bidhaa  zenye  ubora   kuanzia  viwandani  hadi  kumfikia   mlaji.

Wakichangia   kikao  hicho  wafanyabiashara  wanaoingiza  bidhaa  mbali mbali  hapa  nchini   wameiomba     zfda kukaa  pamoja  na   taasisi  za  viwango zbs,mkemia  na  afya   kuwa  na  msimamo  mmoja   wa  kudhibiti   ubara  wa  bidhaa   ili  kuondokana na  mgongano  wa  sheria  uliopo  hivi  sasa .Mkutano  huo  uliowakutanisha wakala  wa  forodha  na  wafanyabiashara wa dawa  chakula  na  vipozi na  vifaa  tiba  wenye  lengo  la  kuwatambulisha wafanyabiashara   mabadiliko  ya  mfumo wa  kiuchumi   kutaka  bidhaa  zote  kupata  ithibati   za  kimataifa   ili  kuingia  katika  masoko  ya  kimataifa.