MABAHARIA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU YA KUSAFISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA

 

Campuni ya danuos  inayosafirisha  mabaharia  zanzibar   imewataka    ma baharia   kuachana   na   kujiunga na biashara haramu ya kusafishaji  wa madawa ya kulevya  ambapo wengi wao wanasadikiwa kufanya biashara hiyo.

akinzungumza   na wafanyakazi   na watendaji  wa meli zinazokwenda nje ya nchi  rais wa campuni hiyo ndugu  ali  mzee yussuf  amesema  mtu  yoyote  atakayekamatwa   na shutuma za madawa ya kulevya campuni  yake haitojihusisha  kwa kumchukulia dhamana   na inapelekea  hata  kuwakosesha ajira baadhi ya wafanyakazi na kusababisha  kufungwa kwa kosa la kusafirisha madawa hayo.

Naye  mkurungenzi  wa kampuni hiyo ndugu  mzee ali  mzee amesema   vijana wengi wanahadaika    na tamaa hali inayopelekea  hata kukosa haki zao za msingin  wanapokamatwa  na  unga  na kuitia dosari kampuni   hiyo   na kuwataka kufata sheria  za kutia mkataba ya kazi,.

Nao wafanyakazi hao wamesema  kuna ubaguzi na kupachikiwa kesi  wanapokuwa wakifanya kazi nje kutokana na ubaguzi wa dini.