MABALOZI WA TANZANIA WANA JUKUMU LA KUITANGAZA NCHI IENDELEE

 

Makamu wa pili wa Raiss wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mabalozi wa tanzania katika mataifa mbalimbali duniani wana jukumu la kuitangaza nchi ili iendelee kuungwa mkono katika kuimarisha uchumi wake.

Amesema yapo maeneo na sekta kadhaa ambazo miundombinu yake iko vizuri kama sekta ya utalii, mawasiliano, kilimo, biashara na afya zinazohitaji kupata msukumo kwa mataifa rafiki na washirika wa maendeleo katika kustawisha uchumi na kuongeza pato la taifa.