MABARAZA YA VIJANA KISIWANI PEMBA YAMETAKIWA KUJIKUSANYA KATIKA VIKUNDI VYA UZALISHAJI

 

Mabaraza ya vijana kisiwani pemba yametakiwa kujikusanya katika vikundi vya uzalishaji na kubuni njia bora zitakazoweza kuwasaidia kuzitumia fursa zilizopo ili  ziweze kuondosha tatizo la ajira linalo wakabili.

Wito huo umetolewa na naibu waziri wa wizara ya vijana sanaa na michezo Mh Lulu Msham wakati  alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya mabaraza ya vijana kisiwani pemba.

Mh Lulu amesema vijana ndio nguvu   kazi ya taifa hivyo hawana budi kuwa na moyo wa kujitolea kwa nguvu zao zote ili kuweza kuleta mafanikio yao pamoja na taifa kwa ujumla

Pia Mh Lulu amewataka vijana hao kuzitumia fursa zilizopo katika shughuli zao pamoja na kuwataka kuwashajihisha na vijana wengine kujiunga na mabaraza ya vijana ili na wao waweze kunufaika

Kwa upande wa vijana hao nao wamesema wanakabiliwa na changamoto mbali mbali za vitendea kazi  ambazo zinawarudisha nyuma katika shughuli zao .