MABINGWA WA TANZANIA BARA, YANGA, IMEFANIKIWA KUWAFUMUA MABINGWA WA COMORO KWA MABAO 5-1

 

 

Mabingwa wa tanzania bara, yanga, imefanikiwa kuwafumua mabingwa wa comoro kwa mabao  5-1 katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya total caf championz  ligi  huko stade de moroni mjini moroni visiwani comoro.

Hadi mapumziko yanga walikuwa mbele kwa mabao 2 – 0.

Bao za yanga yalifungwa na justin zullu, katika dakika ya 43,  saimon msuva dakika ya 45 kabla ya mapumziko.

Mabao mengine yalifungwa na obrey chirwa  dakika ya 59, tambwe dakika ya 65  na kamusoko akamalizia kwenye dakika ya 73 ya mchezo.

Timu hizo zitacheza mchezo wa marudiana jijini dar es salaam wiki ijayo na mshindi kutinga raundi ya kwanza na kucheza na mshindi kati ya zanaco ya zambia na apr ya rwanda ambazo jana zilitoka droo ya  0 – 0 huko zambia.

Mshindi wa hatua hiyo ataenda makundi.

 safari hii makundi ya caf champion  ligi, ambayo  yanajulikana kama total caf champion ligi  yameongezwa kutoka  timu 8 na kuwa timu 16 ambayo yatakuwa na makundi manne ya timu 4 kila moja.

Ni mashindano ya 53 ya kusaka klabu bingwa afrika lakini ni ya 21 tangu mfumo wa caf champion ligi  kuanza.

Mshindi wa mashindano haya atafuzu kucheza mashindano ya fifa ya klabu bingwa duniani yatakayochezwa mwaka 2017 huko united arab emirates na pia kucheza super cup  dhidi ya mshindi wa kombe la shirikisho.

Bingwa mtetezi wa caf championz ligi ni mamelodi sundowns ya afrika kusini.