MABINGWA WAPYA WA TIMU YA BLACK SAILORS NDOGO WAMEREJEA NYUMBANI UNGUJA

 

mabingwa wapya wa daraja la juvenile zanzibar timu ya black sailors ndogo wamerejea nyumbani unguja wakitokea kisiwani pemba katika mashindano ya vijana taifa.

black sailors wamewasili mchana wa leo kwenye bandari ya malindi mjini unguja wakiwa na furaha kubwa baada ya kubeba kombe hilo jana walipoifunga small mkoroshoni united kwa penalty 4-3 kufuatia kumaliza dakika 90 kwa sare ya 0-0.

mbali ya black sailors timu nyengine ilorudi kwao unguja ikitokea huko pemba ni timu ya small real ambao ni makamu bingwa wa daraja la junior baada ya kufungwa jana na lion academy kutoka huko kisiwani pemba kwa penalty 5-4 kufuatia dakika 90 kumalizana kwa sare ya 1-1.

kocha wa black sailors mohd ali (moroco) pamoja na captain wake helef saleh  wamezungumzia siri ya mafanikio mpaka wakatwaa ubingwa huo.nae katibu  mkuu wa soka la vijana wilaya ya mjini juma haji hamza amefurahishwa na vijana wa wilaya yake kwa kubeba kombe hilo.lakini pia zbc ikafanikiwa kuzungumza na abdallah thabit dulla sunday ambae ni katibu wa central taifa na yeye alikuwa na haya ya kuzungumza kuhusu mashindano hayo.