MACRON AAPISHWA KUONGOZA UFARANSA

 

Rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron ameapishwa kuwa rais wa mjini Paris.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 39 ambe ni rais mwenye umri mdogo kuchaguliwa kama rais katika historia ya ufaransa anachukua nafasi hiyo kutoka kwa rais aliyemaliza muda muda wake francois hollande.

Miongoni mwa mambo muhimu katika hotuba yake baada ya kuapishwa ameonesha nia ya kustawisha uchumi wa ufaransa na kukabiliana na hali ya kutoridhisha ya kisiasa.

Hafla hyo ya kiapo inafanyika wiki moja baada ya uchaguzi ambao ulishuhudia ushindi wa mchumi huyo wa kiliberali, mtetezi wa sera za umoja wa ulaya na mpingaji wa sera kali za mrengo wa kulia za marine le pen.