MADAKTARI SABA WA ZANZIBAR WA KUONDOKA TAREHE 15 MWEZI HUU KUELEKEA CUBA

Madaktari saba wa zanzibar wa awamu ya pili waliopata mafunzo kupitia mpango wa masomo ulioasisiwa kati ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar na serikali ya jamuhuri ya cuba wanatarajiwa kuondoka   tarehe 15 mwezi huu kuelekea cuba kwa masomo katika ngazi ya uzamili ya udaktari.

madaktari hao ni miongoni mwa 15 waliopata fursa ya kuendelea na elimu yao ya juu nchini cuba ambao wanane kati yao tayari wanaendelea na masomo kufuatia mkataba uliotiwa saini kati ya zanzibar na cuba mapema mwezi januari mwaka huu hapa zanzibar.

timu hiyo ya madaktari ni pamoja na dr. moh’d mussa, dr. thuwein nassor said, dr. salma hashoul, dr. yussuf said ahmed, dr. khamis suleiman khamis, dr. said khamis ali pamoja na dr. maryam abdullah salim.

akiwaaga madaktari hao wazalendo 7 wa zanzibar ofisini kwake vuga mjini zanzibar makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi alisema azma ya serikali ya kuwapata fursa za elimu zaidi madaktari hao ni kuja kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.

balozi seif alisema taifa limekuwa likitumia gharama kubwa kuwafinyanga watumishi wake lakini baadhi yao wanashindwa kutumnia uzalendo wao na badala yake kuamua kufanyakazi nchi nyengine baada ya kumaliza masomo yao jambo ambalo madaktari hao wanapaswa kuliepuka.

makamu wa pili wa rais wa zanzibar aliishukuru na kuipongeza cuba kupitia ubalozi wake nchini tanzania kwa ukarimu wake wa kupunguza kima cha malipo kwa wanafunzi hao wa fani ya udaktari katika ngazi ya shahada za uzamili ya udaktari.

akitoa salamu zake balozi wa cuba nchini tanzania profesa lucas domingo hernandes alisema zawadi ya masomo waliyopiata wanafunzi hao wapya wa fani ya shahada ya uzalimili ya udaktari wana wajibu wa kuithamini kwa hali zote.

balozi lucas alisema madaktari hao wanapaswa kujizatiti katika kujenga heshima wakati watakaporejea kuendelea na majukumu yao ya kuwapatia huduma bora za afya wananchi  wote.

aliwaasa wanafunzi hao kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote zitakazojitokeza wakati wa  maisha yao mapya ya masomoni ili kujenga heshima ya zanzibar na tanzania kwa ujumla wakiwa kama mabalozi.

naye kwa upande wake waziri wa afya zanzibar mh. hamad rashid mohamed alisema ipo haja kwa kundi hilo kuonyesha mfano mzuri zaidi ya lile lililotangulia masomoni nchini cuba mapema mwaka huu.

waziri hamad alisema serikali wakati inaendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya afya imejenga matumaini makubwa kwa vijana hao ambao watakuwa chachu ya kuimarisha zaidi huduma hizo kwa wananchi wakati wataporejea nchini.

akitoa shukrani kwa serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia wizara ya afya na ubalozi wa cuba nchini tanzania kwa niaba ya wenzake daktari salma hashoul alisema fursa waliotunukiwa ni dhima watakayolazimika kuifanyia haki kwa kujifunza kwa bidii na maarifa.

dr salma alisema ile azma ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar ya kuwateua wao na kuwapeleka mazomoni lazima waifikie kwa ufanisi.