MADIWANI KUANDAA MIKAKATI YA KUFATILIA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA WADI ZAO

Madiwani wa wilaya ya kaskazini “a” wamesisitizwa kuandaa mikakati ya kufatilia miradi ya maendeleo katika wadi zao ili kubaini kasoro za kiutendaji katika utekelezaji wa miradi.
Akifungua kikao cha nne cha bajeti ya baraza la madiwani wa wilaya ya kaskazini “a” mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo mussa ali makame amesema bado juhudi ya kazi ya viongozi hao inahitajika ikiwemo ya kuibua vianzio zaidi vya mapato kwa maslahi ya jamii na taifa zima.
Amefahamisha kuwa mabadiliko hayo yatasaidia pia miradi mingi inayotekeleza kukamailika kwa wakati na kuondosha malalamiko yasiyo ya lazima kwa wananchi.
Katika mkutano huo, muhasibu mkuu wa halmashauri hiyo mtumwa juma omar amesema halmashauri ya wilaya ya kaskazini “a” imefanikiwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato.