MADIWANI KUBUNI MIRADI AMBAYO WATAWEZA KUITEKELEZA NA KUNYANYUA VIPATO

 

Vijana wametakiwa kuwatumia madiwani wao kubuni miradi ambayo wataweza kuitekeleza na kunyanyua vipato vyao ili kuondosha tabia ya kukaa vijiweni ambako kunaweza kusababisha kujiingiza katika viendo viovu.

Wito huo umetolewa skuli ya maendeleo ngwachani na afisa mipango wa baraza la mji mkoani mauwa juma mussa kwa niaba ya mkurugenzi wa baraza hilo rashid abdalla kwenye kongamano la fursa kwa vijana kutoka kwa wadau kwa mabaraza ya vijana ya wilaya hiyo.

Amesema madiwani ni wadau wakubwa wa vijana na wana nafasi kubwa katika kuwasaidia katika shughuli za kimaendeleo kupitia fedha zinazokusanywa katika ofisi yao.

Wawasilishaji wa mada katika kongamano hilo wamesema ushirikishwaji wa vijana katika ngazi mbali mbali za kimaendeleo ni miongoni mwa fursa muhimu wanayostahili kupatiwa.

Washiriki wa kongamano hilo walikuwa na maoni tofauti juu ya mada hiyo.

Nae mjumbe kutoka jukavipe salum abdalla amesema kundi la vijana litakapotengwa uchumi wa nchi utadumaa kwani ndio wadau muhimu katika suala hilo.

Kongamano hilo lililowashirikisha masheha, madiwani, uongozi wa baraza la mji na wa wilaya ya mkoani limeandaliwa na jukavipe kupitia mradi wa kuboresha sera ya maendeleo ya vijana chini ya ufadhili wa shirika la the foundation for civil sosciety.