MADIWANI KUWAHAMASISHA WANANCHI KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YAO

 

Katibu tawala wa wilaya ya kaskazini b nd.makame machano haji amewataka madiwani na viongozi wa halmashauri kuwahamasisha wananchi kufanya usafi ili maeneo yao yawe masafi na waweze kuepukana na maradhi ya mripuko.Wito huo ameutow a huko kiwengwa wakati walipokuwa wakifanya usafi kati maeneo ya fukwe za skuli ya kiwengwa.

Amesema suala la  kufanya usafi ni muhimu kwa kila mtu kuanzia nyumbani ,mwilini na maeneo mengine kwani ndio kudumisha afya za jamii.Mapema kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini b bi.asya moh’d  mzee amesema wamefanya zoezi la usafi katika eneo la kitalii kiwengwa kwa kuionesha mfano jamii ili iweze kufahamu maeneo hayo yanahitaji kufanyiwa usafi kila mara ili yaweze kupendeza na kuvutia watalii kwa ajili yakuongeza kipato kwa taifa.Wakati huohuo nayo jumuiya ya wazaizi ya wilaya ya kaskazini b ikafanya usafi katika kituo cha afya mahonda kwa kuadhimisha wiki ya jumuiya wazazi ambapo makamo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kasakzini b hadia juma chumu akawataka wazazi waitumie wiki hiyo kwa kupinga udahlilishaji.Mwenyekiti wa  hassan sleiman abdalla  na katibusalma shaibu  wa jumuiya ya wazazi ya wilaya ya kaskazini b wamesema wameamua kufanya usafi katika eneo la hospitali kwa kuimarisha afya za wananchi na pia wataendeleza zoezi hilo la maadhimisho ya wiki ya wazazi  kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya wilaya yao.