MADIWANI WA WILAYA YA MKOANI WAMETAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII NA USHIRIKIANO

 

 

Madiwani  wa wilaya ya mkoani wametakiwa kufanyakazi kwa bidii na ushirikiano   kuhakikisha  wanawasimamia ukusanyaji mapato kubuni vyanzo vyengine  vya mapato.

Kauli hiyo imetolewa  na naibu waziri wizara ya nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum za smz  mh,shamata shaame khamis wakati alipokuwa  akizungumza na madiwani wa baraza la mji mkoani  huko katika ukumbi wa ofisi hiyo ikiwa ni miongoni mwa ziara zake  za kujitambulisha  tokea kuteuliwa kwake.

Mh.shamata amesema  katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongeza katika mabaraza ya miji ni kuongeza vyanzo vyengine vya ukusanyaji wa mapato  ili  kuona  lile lengo la uendelezezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi yanafikiwa kwa kiwango kikubwa.

akizungumza katika kikao  hicho mkurugenzi wa baraza la mji mkoani nd.rashid abdalla rashid amesema  watahakikisha malengo ya serikali yanafikiwa katika kubuni miradi inayotekelezeka  kwa wananchi kutokana na mashirikiano wanayoyapata kutoka kwa madiwani hao.

Nae afisa mdhamini wizara ya nchi ,ofisi  ya rais  tawala za mikoa na idara maalum za smz  juma nyasa amewataka madiwani hao kuendelea kupanga mipango madhubuti ya kuhakikisha  mji wa mkoani unakuwa mfano  na kivutio  kwa wageni wanaoingia katika mji huo kutokana na fursa zilizopo.

Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya madiwani  hao wamesema  watahakikisha  wanatumia fursa zilizopo katika kuwendelezaa mji licha ya changamoto inayowakabili ya kutokuwepo mashirikiano baina yao na  viongozi wa majimbo.