MAELEKEZO YA KISHERIA KWA HOTELI KUHUSIANA NA MATUMIZI YA FUKWE NA HIFADHI YA MAZINGIRA YA BAHARI.

 

 

Mkuu wa wilaya ya kati mashavu sukwa ameziagiza idara ya mazingira na kamisheni ya utalii kutoa maelekezo ya kisheria kwa hoteli kuhusiana na matumizi ya fukwe na hifadhi ya mazingira ya bahari.

Agizo hilo la mkuu wa wilaya linatokana na uongozi wa paradise beach resort katika kijiji cha marumbi kuweka kifusi mwanzoni kinyume cha sheria kwa ajili ya kunusuru watumiaji wa fukwe hiyo kudidimia katika tope.

Meneja wa hoteli ya paradise ali mgeni amesema wamechukuwa uamuzi huo kutokana na kuondoa usumbufu kwa wageni wanaofika maeneo hayo lengo likiwa ni kuweka haiba nzuri kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii.

Sheha wa shehia marumbi fumu ali amesema eneo hilo kwa muda mrefu limekua na tope ambapo husababisha watu kudidimia na mchanga uliojikusanya hivi karibuni ulitokana na hoteli hiyo kujenga jeti iliyowekewa mawe mazito.