MAFUNZO JUU YA KANUNI YA KUDHIBITI MATUMIZI YA SIGARA NA TUMBAKU

Wizara ya afya imesema uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi na kwenye sehemu za kutoa huduma za umma si sahihi kutokana na kuathiri afya za wananchi.
Kauli hio imetolewa na afisa mdhamini wizara ya afya pemba bakar ali bakar alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja juu ya kanuni ya kudhibiti matumizi ya sigara na tumbaku yaliyo washirikisha waandishi wa habari, maafisa wa polisi,na wakuu wa mabaraza ya miji na halmashauri huko katika ukumbi wa uwanja wa michezo gombani chake chake pemba.
Wizara imesema imepiga marufuku juu ya matumizi hayo kwa lengo la kupambamba na matumizi ya sigara ili kulinda afya za wananchi.
Akiwasilisha vifungu vya kanuni ya kudhibiti matumizi ya tumbaku zanzibar mratib wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukizika dr omar mwalim omar amesema kwa mujibu wa sheria no.11 ya mwaka 2012 ,sheria ya afya ya jamii na mazingira kifungu namba 109(1) ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuta bidhaa yoyote ya tumbaku au kushika bidhaa hiyo iliyowashwa katika maeneo ya hadhara.
Nao washiriki katika mafunzo hayo wamepata fursa ya kutoa michangao yao .