MAFUNZO KWA MAHUJAJI WANAOTARAJIWA KWENDA MAKKA

 

Jumuiya ya maimamu  kwa kushirikiana na  jumuiya ya ahlaldawa na tahfidhu quan zbar, wameanza kutoa mafunzo  kwa mahujaji wanaotarajiwa kwenda kufanya vitendo vya ibada ya hija huko makka nchini saudi arabia.

akizungumza  baada  ya  semina ,   maalim  khamisi yussuf  kutoka jumuiya  ya maimamu  amesema  lengo   la kutoa mafunzo hayo  ni  kutoa    elimu  kwa watu   wanaokwenda kufanya ibada ya hija.

Amewataka    wananchi wenye uwezo  kuitumia fursa kwa kujitokeza ili kukamilisha nguzo hiyo muhimu katika uislamu.

Amefafanua kuwa mwaka huu  jumuiya zinazosafirisha  mahujaji  zimepewa nafasi nyingi zaidi  ukilinganisha na mwaka  uliopita.

Hata hivyo  malim khamis amesema  mwaka huu mwamko  wa  mahujaji   wanaojiandikisha kwenda  kufanya ibada ya hija umekuwa mdogo  ukilinganisha na mwaka jana.