MAFUNZO YA JKU KULINDA AMANI YA NCHI NA KUWASAIDIA KUJIENDLEZA

 

Vijana wa kujitolea wa jeshi la kujenga uchumi wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo walioyapata kulinda amani ya nchi yao na kuwasaidia kujiendleza kimaisha.

Akifunga mafunzo ya kujitolea ya vijana wa jku  na mafunzo ya  uongozi mdogo wa valantia, waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz  haji omar kheir  amesema taifa linahitaji kuendelea kwa amani iliyopo na kuwa vijana hao wananafasi kubwa ya kulinda amani hiyo.

Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar itahakikisha inawaandaa vyema vijana wake kiulinzi sambamba na kuwajengea uwezo wa kuendesha maisha yao kwa shughuli  mbalimbali zenye tija.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha uuongozi dunga meja khadija ahmada rai amesema  jumla ya vijana 1500 wamemaliza mafunzo yao ambapo wamejifunza kwa vitendo mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali na  ulinzi.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake  bi zawadi vuai salum amesema kutokana na mafunzo walioyapata ni vyema kupatiwa ajira.