MAFURIKO YAWAUA WATU 165 NCHINI INDIA, NEPAL NA BANGLADESH

mafuriko yawaua watu 165 nchini india, nepal na bangladesh.
karibu watu 165 wameuawa na maelfu ya wengine wamehama makaazi yao kufuatia mafuriko makubwa yalitokea nchini nepal, india na bangladesh.
maafisa wamesema kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka wakati kiwango cha uharibifu kikiendelea kubainika.
mvua iliyonyesha siku tatu mfululizo ilisababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi ambayo yamewaua karibu watu 70 nchini nepal, 73 katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa india na 22 nchini bangladesh.
karibu watu 200,000 wanaishi katika kambi za muda katika eneo la assam kaskazini mashariki mwa india.