MAGHARIBI ‘B’ LIMEKABIDHA VIFAA VYA USAFI KWA MABARAZA YA VIJANA

 

 

Wilaya ya magharibi ‘b’ limekabidha  vifaa vya usafi  kwa  mabaraza ya vijana ili vitumike katika uchukuaji wa taka katika maeneo kadhaa ya wilaya hiyo.

Utoaji  wa vifaa hivyo ni mpango wa serikali ya mkoa wa mjini magharibi kuakabiliana na  uchafuzi wa mazingira katika maeneo yote ya mkoa huo ambao ni kioo kwa wageni wanaoingia zanzibar.

Akikabidhi vifaa hivyo mkuu wa wilaya magharibi b kepteni silima haji haji amesema mradi wa taka ni njia  ya kukabilianan na tatizo la kuzagaa kwa taka ovyo mitaani pamoja na kutoa fursa kwa vijana hao kuweza kujiajiri.

Amesema wakati umefika sasa kwa mabaraza ya vijana kuiona changamoto ya kuzagaa kwa taka na wajitume ili kuhakikisha wanarejesha sifa ya zanzibar katikasuala la usafi.

Nao vijana wa baraza la vijina wilaya magharibi b waliokabidhiwa vifaa hivyo wameahid kufanya kila juhudi maeneo yote yanakuwa safi ili kuona mazingira yanakuwa mazuri na kuepukana na maradhi yanayotokana na uchafu.

Mradi wa uchukuaji taka katika wiliya ya magharibi b unazihusisha shehia 36 za wilaya hiyo kupitia mabaraza ya vijana.