MAGUFULI AMEONGOZA KIKAO CHA WAJUMBE WA KAMATI KUU MAALUM YA CCM.

 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm taifa na raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania dr.john pombe magufuli ameongoza kikao cha wajumbe wa kamati kuu maalum ya ccm.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo ya chama cha mapinduzi iliopo lumumba jijini dar es salaam pia kimehudhururiwa  na makamu wa rais samia suluhu hassan, waziri mkuu kassim majaliwa, katibu mkuu wa ccm dr. Bashiru ally, makamu wa pili wa raisi wa zanzibar balozi seif ali iddi na wajumbe wengine.

Pamoja na mengine kikao hicho pia kimemteua ndugu christopher chiza kuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la buyungu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi.