MAHABARIA SABA WA JESHI LA MAJINI PAMOJA NA NAHODHA WAO HAWAJULIKANI WALIPO

Mahabaria saba wa Jeshi la Mjini pamoja na nahodha wao hawajulikani walipo na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya Meli ya kivita ya marekani kugongana na Meli ya Mizigo ya Japan.

msemaji wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako sehemu za ndani zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya manuari hiyo inayoitwa Uss Fitzgerald.

hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino Acx Crystal.