MAHAFALI YA KUMI YA CHUO CHA UWANDISHI WA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA ZANZIBAR

Katibu mkuu wizara ya habari utalii na mambo ya kale Bi Khadija Bakari  Juma amewataka wanafunzi wa chuo cha uwandishi wa habari ambao wamehitimu mafunzo ya stashahada na shahada kuitumia taaluma yao ambayo wameipata chuoni hapo ili kufikia malengo waliojiwekea.

Khadija Bakari ameyasema hayo katika mahafali ya kumi ya chuo cha uwandishi wa habari na mawasiliano ya umma Zanzibar yaliyowajumuisha walimu wa chuo hicho na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali.

Amesema kuhitimu kwa mafunzo hayo sio mwisho wa safari yao kwani sasa wanaingia katika uwanja wa mapambano ya ajira hivyo kuitumia vyema taaluma hiyo kama walivopewa wakiwa madarasani kwani mwandishi mzuri ni yule anaefata sheria na kanuni za habari.

Mkuu wa chuo hicho Ndugu Chande Omar amesema licha ya changamoto zilizokuwepo chuoni hapo lakini anashukuru kwa kufikia hatua nzuri jambo ambalo limeleta mafanikio kwa wanafunzi hao na kufikia lengo walilolikusudia.

Mapema wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo hayo wamesema watajitahidi kuandika habari zilizo sahihi ili kuepusha migongano katika jamii pamoja na kujiajiri na kutosubiri ajira serekalini.

ambapo katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi tisini na nane wamehitimu mafunzo hayo na kukabiziwa cheti na wanafunzi bora wamepatiwa zawadi na mgeni rasmi.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App