MAHAKIMU WAMEPEWA DHAMANA YA KUTEKELEZA NA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI

 

Wakili wa serikali kuu saleh said mubarak amesema mahakimu wamepewa dhamana kubwa ya kutekeleza na kutoa masaada wa kisheria kwa wananchi masikini ili kuwasaidia kupata haki zao kisheriaAkiwasilisha sheria ya msaada wa kisheria katika mkutano wa wadau wa sheria mubarak amesema sheria hiyo inatoa fursa kwa mahakimu kusimamia upatikanaji wamsaada wa kisheria kwa mtu ambae hana uwezo wa kulipia huduma za kuendesha kesi mahakamani

Amefahamisha kuwa ikiwa mtu atakaeshinda kesi atamlipa wakili aliyesimamia kesi yake si zaidi ya asilimia tano ya baada ya kesi yake kutolewa hukumuAmesema mtu aliyepata msaada wa kisheria akishindwa kesi  hatolipa chochote baada ya  kesi yake kutolewa hukumu kuwa ameshindwa

Hata hivyo amewataka mahakimu kusimamia vizuri dhamana hiyo ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa Nao washiriki wa mkutano huo wameiomba serikali kuweka chombo maalumu cha kusimamia mfuko wa fedha za uendeshaji wa sheria hiyo