MAITI IMEOKOTWA KATIKA UKANDA WA BAHARI YA KUSINI

Matukio ya kuokotwa watu waliofariki pembezoni mwa fukwe za bahari ya zanzibar yameendelea baada ya maiti nyengine kuokotwa katika ukanda wa bahari ya kusini.
Hiyo ni maiti ya nne kuokotwa katika kipindi kisichozidi wiki moja ikiwa katika mazingira ya vifo vinavyofanana kwa kufungwa mpira shingoni na kuzongwa mifuko ya plastiki pamoja na kuwa na majeraha makubwa.
Maiti hiyo imeokotwa imekutwa imefungwa mikono kwa nyuma kwa kamba huku tayari ikiwa imeharibika vibaya pia imekosa kutambulika .
Kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja juma saad akizungumzia matukio hayo amesema ni ya kutisha na huenda yanafanywa kwa lengo maalum na watu wasiojulikana.
mkuu wa wilaya ya kusini idrissa kitwana mewataka wananchi kuwa makini na kutoa ushirikiano kila wanapoona viashiria vya uhalifu pamoja na watu wasiowafahamu katika maeneo ya.o.