MAJAJI NCHINI KENYA WAMEPINGA KAULI ZA VITISHO ZILIZOTOLEWA NA RAIS UHURU KENYATTA

Majaji nchini kenya wamepinga kauli za vitisho zilizotolewa na rais uhuru kenyatta baada ya mahakama kuu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini humo agosti 8. Na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini.
Baraza la mahakama na jumuiya ya majaji nchini humo wamewataka wananchi wa kenya kupuuza kauli hizo za wanasiasa kwa vile uamuzi huo wa kufuta matokeo umetolewa na majaji huru.
Rais kenyatta amesema taifa hilo lina ‘matatizo’ na idara ya mahakama ambayo pia ina matatizo inahitaji marekebisho. Na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi huo wa mahakama.